Chagua lugha:

SIKU YA USHAIRI WA WATOTO

Siku ya Ushairi wa Watoto Duniani (WoChiPoDa) ilianzishwa mwaka 2014, wakati mwandishi na mshairi Gloria D. Gonsalves aliamua kuchukua hatua juu ya wazo alilolipata wakati akitembea kwenye msitu wa Altenberg, Ujerumani. Kwanza, alifikiri ni wazo la kuandika shairi. Hata hivyo, miti mirefu iliyofunikwa na kijani ya ajabu haikuwa tayari na wazo la uandishi wa shairi. Baada ya masaa mawili ya kutembea, aliandamwa na WoChiPoDa.

  • Siku ya Ushairi wa Watoto.
  • Jumamosi ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Ushairi wa Watoto. Siku hii watoto hujifunza mashairi katika mazingira yanayoleta burudani.  Pia, watoto wataghani mashairi waliyoandika wenyewe. Wasikilizaji wanaweza kuwa ni familia, marafiki, wanafunzi, walimu au mtu mwingine yeyote.
  • Andika shairi kuhusu mada iliyotolewa.
  • Kuwa huru kuchagua mada nyingine kuendana na mazingira yako.
  • Kusanya watu unaotaka wasikilize shairi lako.
  • Soma shairi lako.
  • Mpe shairi lako msikilizaji yoyote unayetaka aliweke kama kumbukumbu.
  • Mashairi ni burudani!
  • Shiriki kwa kutuma picha, video na mashairi kwenye ukurasa wetu wa mtandaoni.
  • Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya maandalizi, soma hapa.