Chagua lugha:

SIKU YA USHAIRI WA WATOTO

Siku ya Ushairi wa Watoto Duniani (WoChiPoDa) ilianzishwa mwaka 2014, wakati mwandishi na mshairi Gloria D. Gonsalves aliamua kuchukua hatua juu ya wazo alilolipata wakati akitembea kwenye msitu wa Altenberg, Ujerumani. Kwanza, alifikiri ni wazo la kuandika shairi. Hata hivyo, miti mirefu iliyofunikwa na kijani ya ajabu haikuwa tayari na wazo la uandishi wa shairi. Baada ya masaa mawili ya kutembea, aliandamwa na WoChiPoDa.

 • Siku ya Ushairi wa Watoto.
 • Jumamosi ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Ushairi wa Watoto. Siku hii watoto hujifunza mashairi katika mazingira yanayoleta burudani. Watoto wataghani mashairi waliyoandika wenyewe. Wasikilizaji wanaweza kuwa ni familia, marafiki, wanafunzi, walimu au mtu mwingine yeyote. Na yote haya hufanyika karibu na moto mkubwa, fanusi au mishumaa. Hii kama si burudani, ni nini?
 • Andika shairi kuhusu kitu chochote.
 • Tafuta mtu mzima wa kukusaidia na maandalizi.
 • Washa moto, fanusi au mishumaa (hii ni hiari). Kuwa huru kuchagua mada ya sherehe k.m. mazingira, wanyama, mimea, n.k.
 • Kusanya watu unaotaka wasikilize shairi lako pembeni ya moto au mishumaa.
 • Soma shairi lako.
 • Mpe shairi lako msikilizaji yoyote unayetaka aliweke kama kumbukumbu.
 • Mashairi ni burudani!
 • Shiriki kwa kutuma picha, video na mashairi kwenye ukurasa wetu wa Facebook au Instagram.
 • Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya maandalizi, soma hapa.